Home Habari za michezo YANGA NA MTIBWA KESHO VITAUMANA…..MASTAA HAWA ‘KUPAPATUANA’…

YANGA NA MTIBWA KESHO VITAUMANA…..MASTAA HAWA ‘KUPAPATUANA’…

Habari za Yanga

YANGA kesho inashuka dimbani ikiwakaribisha Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa katika uwanja wa Azam, uliopo Chamazi Dar-es-Salaam saa 1:00 usiku.

Katika mchezo huo Yanga inahitaji alama tatu muhimu ili kurejea kileleni, wakishinda leo watakuwa nafasi ya pili wakicheza michezo tisa na akikusanya alama 27, akishinda leo atakuwa na pointi 24 na Azam FC wakiongoza ligi wakiwa na pointi 28 wakiwa na michezo 12.

Huku Mtibwa Sugar ambao wanahitaji kujinusuru kutoka mkiani na kupambana wanafanikiwa kuvuna alama muhimu mbele ya wenyeji wao Yanga.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema baada ya safari ndefu kutoka Ghana, walitumia muda mzuri wa kujiandaa kwa mchezo wao wa leo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Amesema amefanya maandalizi mazuri na kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya kuvuna alama tatu katika mchezo huo ugumu kulingana na alivyowaona wapinzani wake Mtibwa Sugar ambao hawana matokeo mazuri.

“Kikosi kipo tayari kuwavaa Mtibwa Sugar, kufanya mzunguko wa wachezaji wake anachoangalia zaidi ni juhudi Mchezaji wachezaji, ukiangalia viungo wamekuwa wakifanya vizuri na kufunga idadi kubwa ya mabao kuliko washambuliaji kwa hali ambayo inamlazimu

Timu imecheza michezo mechi 18 timu imefunga mabao 40, viungo watatu wa juu wamefunga mabao 25, Maxi Nzegeli (8), Pacome Zouzoua (7) na Aziz Ki (8), watu wanataka nibadili na kutumia mawinga je kati ya viungo hao nani nimtoe na kuwapa nafasi mawinga.

Pia kwenye viungo wakabaji wengi lakini kati ya hao Khalid Aucho ameonyesha uwezo mkubwa je kati ya Zawadi Mauya, Mudathiri Yahya, Salum Abubakari na Jonas Mkude amtoe nani ili aweze kufanya mzunguko ambao wanaowaka mashabiki,” alisema Gamondi.

Ameongeza kuwa mechi ya Ihefu FC alifanya mabadiliko ya kikosi lakini walipoteza , hawezi kufanya mabadiliko lakini hawezi kubadilisha timu yake ya ushindi na kulazimika kuwapa nafasi wachezaji ambao wanapambana na kumpa matokeo mazuri.

Naye kipa wa Yanga, Abdultwalib Mshery amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanaendelea walipoishia katika kuvuna alama tatu katika kila mchezo.

“Tunaenda kupambana kuhakikisha tunavuna pointi tatu dhidi ya Mtibwa Sugar, hautakuwa mechi rahisi na tutacheza kwa nidhamu ya hali ya juu,” amesema Mshery.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema wamejipanga vizuri na anaamini hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu ya kutokuwa na matokeo mazuri katika mechi zilizopita.

Amesema anahitaji matokeo mazuri katika mechi yao dhidi ya Yanga ambayo anahitaji matokeo chanya ili kurejesha morali ya timu na kujiweka kwenye nafasi nzuri.

“Presha ipo kwa kila upande, tumewapa maelekezo wachezaji wetu jinsi ya kucheza dhidi ya Yanga, lakini tukiingia kwa nidhamu ya hali ya juu ili kufikia malengo yetu.

Licha ya kuwafunga Yanga nikiwa Ihefu FC, lakini sasa hivi naenda kivingine kwa sababu Mtibwa Sugar inahitaji matokeo mbele ya Yanga kuliko kitu kingine ,” amesema Katwila.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WAIVORY...MO DEWJI AKUNJUA POCHI SIMBA....ATOA AHADI YA MAMILIONI..BOCCO AJIFUNGA ULIMI..