Home Habari za michezo EE BWANA!! MAYELE AWEKA REKODI HII MPYA YA KIBABE…AMEZUNGUMZA HAYA

EE BWANA!! MAYELE AWEKA REKODI HII MPYA YA KIBABE…AMEZUNGUMZA HAYA

EE BWANA!! MAYELE AWEKA REKODI HII YA KIBABE...AMEZUNGUMZA HAYA

Nimeweka rekodi! hii ni kauli ya kinara wa upachikaji wa mabao Kombe la Shirikisho Afrika (5) na Ligi Kuu Bara (16), Fiston Mayele ambaye amefanikiwa kufunga mabao 50 ndani ya msimu mmoja na nusu tangu amejiunga na Yanga, huku akisema bado anataka kufanya makubwa zaidi.

Mayele juzi alifanikiwa kuonyesha kiwango cha juu na kufunga mabao mawili dhidi ya Rivers United hali iliyomfanya afikishe mabao 50 ambayo ameyafunga katika mashindano yote ya ushindani tangu ametua Yanga.

Akizungumza nasi, Mayele raia wa DR Congo alisema ameweka rekodi ambayo haitasahaulika kwenye maisha yake ya soka huku akitumia nafasi hiyo kuwashukuru wachezaji wenzake, benchi la ufundi na viongozi kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuitumikia Yanga.

“Nimeweka alama kwenye soka la Tanzania, namshukuru sana Mungu pia kwa kunipa afya njema, namuomba aendelee kunipa uhai zaidi ili niendelee nilipoishia sasa bado nina mechi nyingi mbele natamani kuona nafunga mabao zaidi ya haya 50 ambayo nimeyafunga, nafikiri bado nina kazi kubwa ya kufanya huko mbele.” alisema Mayele ambaye yupo kileleni kwenye chati ya mabao Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi Kuu.

Alisema mchango mzuri anaoupata kutoka kwa wachezaji wenzake ndiyo siri ya mafanikio hayo huku akisisitiza kuwa ataendelea

kutumia kila nafasi atakayoipata ili kuendelea kuweka rekodi nzuri na bora ndani ya kikosi cha Yanga.

“Ukweli tangu nimekuja hapa nchini nimepata ushirikiano wa kutosha kwa wachezaji wenzangu, benchi la ufundi na hata viongozi hii ndiyo imenifanya nifike hapa nilipo leo.

Akizungumzia mchezo wao dhidi ya Rivers United, Mayele alisema ulikuwa mchezo mgumu na wa ushindani kwa timu zote mbili walitengeneza nafasi nyingi na kufanikiwa kutumia mbili ambazo zimewapa mwanga kuelekea hatua ya nusu fainali.

“Timu zote zilijiandaa vyema lakini sisi tulikuwa bora na ndio maana tumepata matokeo ambayo yametupa mwanga wa kuweza kujihakikishia nafasi ya nusu fainali kama tutafanya vizuri nyumbani;

“Benchi la ufundi na wachezaji kwa ujumla lengo ni kuvuka hatua inayofuata tutapambana dakika 90 zilizobaki ili kupata matokeo ya ushindi na kukamilisha kisasi cha msimu uliopita ambapo Rivers walitufunga nyumbani na ugenini.” alisema.

Mayele alisema wameshasahau matokeo yaliyopita wanarudi kujiweka sawa tayari kwa kumkaribisha Rivers Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na timu hiyo inatua alfajiri ya leo.

MABAO YA MAYELE 2021/22 Ligi Kuu alifunga mabao 16 Kombe la Shirikisho (ASFC) 2 Ngao ya Jamii 1 2022/2023 Ngao ya Jamii 2 Ligi Kuu Bara 16 ASFC 1 ligi ya Mabingwa 7 Kombe la Shirikisho 5

SOMA NA HII  GAMONDI AMEKUNA KICHWA KUHUSU KONKONI KISHA ASEMA HAYA