Home Simba SC STRAIKA MKONGO ANATUA KUKAMILISHA DILI LA KUJIUNGA NA SIMBA

STRAIKA MKONGO ANATUA KUKAMILISHA DILI LA KUJIUNGA NA SIMBA


MSHAMBULIAJI wa DC Motema Pembe ya nchini DR Congo, Kadima Kabangu amefunguka kuwa tayari ameshamalizana na Simba na wiki hii kila kitu kitakuwa sawa tayari kwa kutangazwa kuwa mchezaji rasmi wa Simba.

Kadima Kabangu kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba, ambao kwa sasa wametimkia Morroco ambapo wameenda kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa mashindano yote.

Akizungumzia dili hilo, Kabangu amesema kuwa kwa sasa meneja wake yupo katika mazungumzo ya mwisho kumalizana na Simba hapa Tanzania, huku mwenyewe akiweka wazi kuwa anatarajia kutua nchini wiki hii kwa ajili ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Simba.

“Meneja wangu yupo Tanzania kwa sasa, amesema kuwa wiki hii kila kitu kitakuwa sawa, kuhusu mimi kuja Tanzania nimeambiwa wiki hii nitasafriki kuja huko hivyo nasubiri taarifa hiyo lakini ni uhakika.

“Tayari nimehakikishiwa na kocha wa Simba Didier Gomes kuwa nipo kwenye mipango yake ya kuitumikia Simba, kwa ajili ya msimu ujao, hivyo naamini hilo ndio linaenda kutokea,”amesema mshambuliaji huyo.

SOMA NA HII  KWELI SIMBA NI LEVEL ZINGINE...WAPITIA ULAYA KUWAFUATA WAMOROCCO...KUWEKA KAMBI YA KISHUA...