Home Uncategorized TIMU YA MBWANA SAMATTA YAAMBULIA POINTI MOJA

TIMU YA MBWANA SAMATTA YAAMBULIA POINTI MOJA

ASTON Villa ya Mbwana Samatta leo imelazimisha sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa dhidi ya Sheffield United.

Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo kipindi cha kwanza liliibuka tukio la aina yake baada ya kipa wa Aston Villa kusukumwa na mchezaji wake kisha kuingia na mpira ndani ya eneo la lango lake ila halikuwa goli kwa mujibu wa mwamuzi na teknolojia ya goli haikuweza kulitambua.

Nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta aliingia uwanjani kipindi cha pili na kuonyesha makeke yake kiasi kidogo akitumia dakika 21 uwanjani.

Aliingia dakika ya 68 akichukua nafasi ya Trezeguet.

SOMA NA HII  YANGA YAUZIWA MBUZI KWENYE GUNIA