Home news RAIS SAMIA AFANYA KWELI YANGA..AONGEA ‘LIVE’ NA MANARA..ACHANGA MAMILIONI YA PESA…GSM AUNGA...

RAIS SAMIA AFANYA KWELI YANGA..AONGEA ‘LIVE’ NA MANARA..ACHANGA MAMILIONI YA PESA…GSM AUNGA MKONO…


RAIS wa Tanzania Samia Suluhu ameahidi kutoa kiasi cha Sh15 milion kwa taasisi ya mtoto Ali Kimara (10) ambaye amekuwa akisumbuliwa na changamoto ya upumuaji kwa takribani miaka 8 sasa.

Mbali na Rais Samia wengine waliochangia taasisi hiyo ni GSM ambaye ametoa kiasi cha Sh10 milioni.

Ali amekuwa akitumia mashine ya umeme kumsaidia kupumua masaa 24 ama kuwekea mtungi wa gesi pale umeme unapokatika.

Jana katika uwanja Chamanzi kabla ya mechi ya kirafiki kati ya Yanga na timu ya taifa ya Somalia, Rais Samia akizungumza kwa njia ya simu na msemaji wa Yanga, Haji Manara ameahidi kuchangia fedha hizo kwa taasisi hiyo inayojishughulisha na kuwasemea watoto wote wenye magonjwa adimu yasiyo na tiba ambayo kwa sasa yapo zaidi ya 7000 duniani.

“Suala hili la magonjwa adimu tumeangaika nalo muda sasa tunafurahi kuona Yanga wamelifikisha kwa umma na mimi kwa kuunga mkono naahidi kutoa kiadi cha Sh15 milioni kuisaidia taasisi hiyo,” amesema Rais Samia

Akizungumza uwanjani hapo mama mzazi wa Ali, Sharifa Mbarak amesema lengo la taasisi hiyo ni kuwasemea watoto wenye magonjwa adimu ili kuwafikia watunga sera, wafanya maamuzi pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusiana na magonjwa hayo adimu.

Amesema anamshukuru Rais Samia na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi kwa kuendelea kuwaunga mkono kuhakikisha watoto wenye magonjwa hayo adimu wanapata tiba.

“Milioni 10 na 15 tulizozipata hapa zitaelekea moja kwa moja kwaajili ya kuanza tafiti kwa ajili ya magonjwa adimu lengo kujua ni kwa kiwango gani magonjwa haya yapo hapa nchini,” amesema

Mbarak amesisitiza kuwa tayari wameshaanza maongezi na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Idara ya Tafiti (Muhas) kwa ajili ya kuanzisha tafiti za magonjwa hayo adimu nchini Tanzania.

SOMA NA HII  KUHUSU MECHI ZA SIMBA NA YANGA...NABI KAVUTA HISIA WEEE..KISHA KWA UPOLE KASEMA HAYA..