Home Uncategorized SERGIO RAMOS AOMBA KUTIMKIA CHINA

SERGIO RAMOS AOMBA KUTIMKIA CHINA


SERGIO Ramos ambaye ni nahodha wa kikosi cha Real Madrid amecheza jumla ya michezo 606 akiwa ndani ya kikosi hicho tangu ajiunge kwenye kikosi hicho msimu wa mwaka 2005/06 na sasa ameomba kusepa kikosini hapo.


Ramos amewaeleza viongozi wa kikosi hicho kuwa amepata dili la maana kwenye moja ya timu nchini China hivyo hamna namna ya yeye kubaki kikosini hapo.

Imeelezwa kuwa amefikia uamuzi huo kutokana na kutoelewana na Rais wa klabu hiyo Florentino Perez kutokana na lawama anazotupiwa kwamba anahusika kwenye kuboroga kwa kikosi hicho.
SOMA NA HII  STRAIKA MAN UNITED ATUA INTER MILAN