Home Habari za michezo KAMWE:- HESABU ZA YANGA CAF ZIMENYOOKA….MWARABU LAZIMA AFIE KWA MKAPA…

KAMWE:- HESABU ZA YANGA CAF ZIMENYOOKA….MWARABU LAZIMA AFIE KWA MKAPA…

Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe

Klabu ya Yanga imesema kuwa baada ya kutinga hatua ya makundi kwenye michuano ya CAFCL, sasa wanaitaka robo fainali ya michuano hiyo mikubwa Barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ally Kamwe wakati akitangaza uzinduzi wa hamasa kuelekea mchezo wao wa marejeano dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria utakaopigwa Jumamosi ijayo Februari 24, 2024 katika Dimba la Mkapa na kuupa mchezo huo jina la ‘Pacome Day Kitaalam Zaidi’.

“Naamini kila mmoja wetu anafahamu ugumu wa kundi tulilopo na nini tunatakiwa tufanye ili kufuzu kwenda hatua ya robo fainali. Ugumu wa kundi letu ni kwamba hakuna mbabe wala mnyonge, kila mmoja ana nafasi ya kwenda robo fainali.

“Ahly ana alama sita, CR alama tano, Yanga alama tano na Medeama alama nne, kwa hiyo yeyote atakayeshinda mechi zake mbili na kupata alama zote sita ana nafasi ya kuingia hatua ya robo fainali.

“Sisi Yanga hesabu zetu zimenyooka kama rula, hii ni kwa sababu tukipata alama tatu za CR Belouizdad, asilimia 70 tutakuwa tumetumbukia hatua ya robo fainali. Hatujafika muda wa kupiga ramli upande wa Medeama na Ahly nini kitatokea.

“Sisi Yanga, akili yetu, nguvu yetu, maaraifa yetu na ujuzi wetu wote ambao Mungu ametujalia tuuelekeze kwenye mchezo huo ambao umebeba asilimia kubwa ya kutupeleka makundi. Mwarabu anatakiwa afe kwa Mkapa, hakuna stori nyingine, Mwarabu lazima afe,” amesema Ally Kamwe.

SOMA NA HII  IMEFICHUKAA...HIVI NDIVYO USAJILI WA 'SURE BOY' ULIVYOIKAMUA YANGA MAMILIONI YA PESA...