Home Uncategorized AZAM FC WALITAKA KOMBE LA SIMBA MAPEMA

AZAM FC WALITAKA KOMBE LA SIMBA MAPEMA


 AZAM FC imesema kuwa malengo makubwa kwa msimu huu ni kushinda kila mechi ili kupata pointi tatu muhimu zitakazowapa nafasi ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara mapema.

 

Azam FC inaongoza msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi nne, huku ikishinda michezo yote na kukusanya pointi 12, ambapo Simba inayoifuata ikiwa na pointi 10 na Yanga ina pointi 10 pia zikiwa zimetofautiana katika idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.


Kwa sasa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ni Simba ambao walitwaa taji hilo msimu uliopita nao wanapambana kuweza kulitwaa tena sambamaba na Yanga ambao nao wameweka wazi malengo yao ni kusepa na taji hilo.

 

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’ amesema kuwa, Azam imejipanga kuhakikisha inafanikiwa kushinda michezo yao yote ili kuendelea kubaki namba moja.


“Azam msimu huu tumejipanga kuhakikisha tunachukua kombe, tumeshajua mapungufu ambayo yalikuwa yakijitokeza katika baadhi ya mechi zetu hasa zile za mikoani ambapo wachezaji wamekuwa wakifanya mazoezi katika viwanja viwili tofauti cha nyasi bandia na cha vumbi.

 

“Tumejipanga kuhakikisha tunafanikiwa kuibuka na pointi tatu muhimu katika kila mechi tutakayocheza na ikitokea iwapo tumepoteza ni kwa bahati mbaya, lakini tunahitaji ushindi mnono, mwalimu anatumia muda wake vyema kukipanga kikosi chake,” amesema Zaka Zakazi. 


Kwa sasa kikois kinajipanga kwa ajili ya mchezo wa raundi ya tano dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 1:00.

SOMA NA HII  LUSAJO MTAMBO WA MABAO NDANI YA NAMUNGO UNAOHUSISHWA KUJIUNGA YANGA