Home Habari za michezo HUYU HAPA DOGO MTZ ALIYEPATA SHAVU LA KUCHEZA LIGI MOJA NA MESSI...

HUYU HAPA DOGO MTZ ALIYEPATA SHAVU LA KUCHEZA LIGI MOJA NA MESSI WA PSG…

Mshambuliaji Mtanzania, Omar Abbas Mvungi aliyekuwa kwenye mpango wa Garuda Select 4 nchini England, ameula Ufaransa baada ya kusainishwa mkataba wa kukipiga Klabu ya Nantes, akiwa mchezaji wa kwanza kutoka nchini kujiunga na timu inayoshiriki Ligue 1.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ufaransa, kinda huyo mwenye umri chini ya miaka 20 atakuwa na timu ya vijana ya kikosi hicho kwa ajili ya kuendelezwa.

Omar ameonyesha furaha yake kufuatia kukamilika kwa uhamisho huo kwa kusema:”Huu ni wakati wa kujivunia sana kwangu na kwa familia yangu. Nimefurahi kusaini mkataba wangu wa kwanza kama mchezaji wa kulipwa na FC Nantes.

“Ni heshima kubwa kuwa katika klabu ya ajabu kama hii. Nataka kumshukuru kila mtu ambaye ameshiriki kusaidia kufanikisha hili. Ninapitia safari ndefu hadi sasa. Nasubiri kwa hamu kuanza majukumu yangu.”.

Wakati akiwa Tanzania, Omary alikuwa kwenye kituo cha kuibua na kukuza vipaji cha Cambiasso kabla ya kwenda England na baadaye Jamhuri ya Czech ambako aliichezea MFK Vyskov ambayo wachezaji wengi wa Kitanzania wamepita akiwemo Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

SOMA NA HII  KAMWAGA: SIMBA NA PABLO FRANCO; HATUA MOJA TU LAKINI HATUA KUBWA SANA...