Home Azam FC NYOTA SABA WA AZAM FC WAITWA TIMU YA TAIFA

NYOTA SABA WA AZAM FC WAITWA TIMU YA TAIFA


KLABU ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina imetoa jumla ya wachezaji 7 ambao wameitwa kwenye timu mbalimbali za taifa.

 Wachezaji hao saba tayari wamesharipoti timu mbalimbali za Taifa, kwa ajili ya mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwakani 2022 nchini Qatar.

Ni kiungo Idd Seleman ‘Nado’, Edward Manyama, Lusajo Mwaikenda na Wilbol Maseke, wameripoti timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Kiungo Kenneth Muguna, ameenda kujiunga na timu yake ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ huku nahodha msaidizi, Bruce Kangwa na kiungo Never Tigere, hawa wameripoti timu ya Taifa ya Zimbabwe ‘Warriors’.

Kocha wa viungo, Nyasha Charandura, naye ameripoti timu ya Taifa ya Zimbabwe.

Azam FC inanawatakia kila la kheri katika majukumu yao ya timu za Taifa.

SOMA NA HII  A-Z JINSI SIMBA ILIVYOIFANYIA UMAFIA RUVU SHOOTING JANA....YANGA WAJIBIWA KIBABE....