Home Uncategorized KOCHA SIMBA AWAVAA WACHEZAJI

KOCHA SIMBA AWAVAA WACHEZAJI


Kocha wa klabu ya Simba, Sven Vandenbroeck, amesema hajaridhishwa na uwezo wa safu yake ya ulizi baada ya mechi ya Kombe la FA dhidi ya Mwadui FC.

Kocha huyo alisema licha ya kufanikiwa kutinga kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la FA baada ya kuwang’oa Mwadui kwa mabao 2-1 kwenye mchezo ulichezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam bado anafikiria kuja na dawa itakayosaidia kuzuia hali hiyo.

“Tumepata ushindi kwenye mchezo wa leo (juzi) na tumefanikiwa kusonga hatua inayofuata ni jambo nzuri kwa timu, lakini kwangu binafasi bado sijafurahishwa na safu yangu ya ulinzi katika michezo minne iliyopita kila mechi tumeruhusu kufungwa bao na kinachoniumiza kichwa zaidi ni namna wanavyofungwa, “ alisema Sven.

Simba ukitoa mchezo dhidi ya Mwadui mechi zingine tatu ambazo Simba imefungwa licha ya ya kuibuka na ushindi ni pamoja na Alliance 4-1, mbele ya Mbao 2-1 na ule waliotaka sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Yanga.

Alisema kinacho muumiza kichwa ni namna safu ya ulinzi inavyoruhusu kufungwa ni kutokana na kukosa mawasiliano na wakati mwingine wakishafungwa wanakuwa kwenye presha kubwa ya kutengeneza mazingira ya kutafuta bao la kusawazisha.

Sven alisema kwenye mchezo huo kuanzia sehemu ya kiungo walicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi za kupata mabao lakini kukosekana kwa umakini sehemu ya mwisho ilisababisha kuchukua muda mrefu hadi kufanikiwa kupata bao la ushindi kupitia Francis Kahata.

SOMA NA HII  KUHUSU MCHEZAJI BORA WA MWEZI YANGA MCHAKATO UKO HIVI