Home Uncategorized ISHU YA TOYOTA IST YA KABWILI YAPAMBA MOTO, SIMBA KUTOA TAMKO LEO,...

ISHU YA TOYOTA IST YA KABWILI YAPAMBA MOTO, SIMBA KUTOA TAMKO LEO, TFF YAPIGILIA MSUMARI


UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo utalitolea ufafanuzi suala la madai ya mlinda mlango wa Yanga, Ramadhan Kabwili kudai kuwa aliahidiwa gari aina ya Toyota IST endapo angefanya makusudi ya kutocheza mchezo wao wa msimu uliopita 2018/19.

Kabwili alidai kuwa, kuna watu ambao anadai walikuwa ni viongozi wa Simba walimfuata na kumtaka afanye makusudi kwenye mechi zake apate kadi ya njano ili asipangwe kwenye kikosi kwa kuwa alikuwa na kadi mbili za njano.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa watajibu tuhuma alizotoa mchezaji huyo ila cha msingi awe na ushahidi.

” Tutajibu tuhuma za jumla jumla alizotoa huyu mchezaji kwa klabu yetu. Muhimu wakati huu akijiandaa kikamilifu na ushahidi wa hizo tuhuma,” .

Shirikisho la Soka la Tanzania, (TFF) limetoa pia taarifa ya kusikitishwa na taarifa hizo kwa kuwa si mpango mzuri kwa maendeleo ya soka na wameahidi kulifanyia uchunguzi.

“Sektretarieti ya TFF imeiandikia barua Kamati ya Maadili kufuatilia jambo hilo ikiwa pamoja na kufahamu undani wa jambo lenyewe.

“Aidha TFF, itavijulisha vyombo vingine vya usalama ili viweze kuisaidia uchunguzi kubaini ukweli na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

“TFF siku zote imekuwa ikipiga vita vitendo vya upangaji matokeo katika mpira wa miguu,” ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa na TFF kupitia Ofisa Habari, Cliford Ndimbo. 

SOMA NA HII  NAMUNGO YAPANIA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA