Home Uncategorized SAMATTA ANAAMINI WATANZANIA WOTE WATAMPA SAPOTI

SAMATTA ANAAMINI WATANZANIA WOTE WATAMPA SAPOTI


MBWANA Samatta, nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania anayekipiga Klabu ya Aston Villa amesema kuwa kutua kwake ndani ya Aston Villa kutaungwa mkono na watanzania wengi watakaoishabikia timu hiyo.

Samatta amesaini dili la miaka minne na nusu ndani ya Aston Villa akitokea Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Ni mchezaji wa zamani wa timu ya African Lyon, Simba ndani ya Bongo na TP Mazembe ya Congo ni mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kusajiliwa na timu inayoshiriki Ligi Kuu England.


 “Ilikuwa ni maombi yangu ya muda mrefu na ndoto zangu kucheza Ligi Kuu ya England na tangu nikiwa mdogo nilikuwa nikiitazama ligi hii kwenye TV na Aston Villa ni miongoni mwa timu nilizokuwa nazitama. Kuja kwangu hapa ninaamini nitapewa sapoti na mashabiki wangu wa Tanzania,” amesema.

Aston Villa leo itakuwa na kibarua mbele ya Leicester City wakiwa nyumbani ikiwa ni mchezo wa FA, Dean Smith, Kocha Mkuu wa Villa amesema kuwa Samatta anaweza kuanza leo.

Aston Villa wanatakiwa kushinda mechi ya Leo ili kusonga mbele baada ya mchezo wa Kwanza kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1.

SOMA NA HII  HAPO SIMBA NI FULL MZIKI, BOCCO AFUNGUKA