Home news NABI – YANGA PANA UKAME…AFUNGUKA HALI ILIVYO A-Z..ATAJA SIRI MBILI ZA UBINGWA….

NABI – YANGA PANA UKAME…AFUNGUKA HALI ILIVYO A-Z..ATAJA SIRI MBILI ZA UBINGWA….


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nesreddine Nabi amefichua kitu juu ya ushindani wa Ligi Kuu Bara huku akitaja siri kuu mbili zinazoweza kuwabeba kutwaa taji msimu huu.

 Yanga ndio vinara wa ligi hiyo baada ya kucheza michezo 14 ya mzunguko wa kwanza na kukusanya pointi 36 wakiwa mbele pointi tano na watani zao Simba walio nafasi ya pili na pointi 35.

Akizungumza na gazeti la  Mwanaspoti, Nabi alisema ameangalia misimu minne ambayo timu yake imesota bila kutwaa taji lolote na kujipiga kifua kuwa yeye ni bora na ana nafasi nzuri ya kufanya vizuri.

“Yanga wana ukame wa kutwaa taji ndani ya misimu minne nimefuatilia na nimebaini mapungufu ndani ya misimu hiyo ni ufinyu wa kikosi na kukosa mastaa wenye mwendelezo wa ubora kitu ambacho msimu huu anacho,” alisema na kuongeza;

“Nafurahi msimu huu nimeikuta timu nzuri na ina kikosi kipana ambacho akikosekana mmoja mwingine anachukua nafasi na anafanya kile kinachotakiwa kufanywa,” alisema.

Alisema Yanga ya msimu huu imekuwa na mfululizo wa majeruhi lakini hakuna pengo linaloonekana tofauti na misimu iliyopita na aliongeza kuwa mastaa wake wana ari ya ushindani.

“Timu sasa inaweza ikatanguliwa kufungwa wachezaji wakarudi mchezoni na kusawazisha hadi mpira unamalizika wanaongeza bao la ushindi tofauti na nyuma alivyoifuatilia timu hiyo,” alisema.

Akizungumzia ishu ya kutoka sare kama imewaondoa mchezoni alisema hawana sababu ya kufanya hivyo kwa sababu bado wanamichezo mingi mbele, hivyo wanapambana kuhakikisha wanarekebisha walipokosea ili waweze kusonga mbele.

Alisema wanaongoza ligi wanahitaji kuendelea hivyo hadi mwisho wa msimu hivyo hawahitaji kumfikiria zaidi anayewakimbiza zaidi ni kupambana kupata matokeo kila mchezo huku akiitaja Mtibwa Sugar kuwa ndio timu inayompa wakati mgumu kwani wanaenda ugenini.

Yanga mchezo wake wa mwisho wa ligi waliambulia suluhu na Mbeya City na wanatarajia kuwa ugenini Februari 23 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro.

SOMA NA HII  WAAMUZI WA YANGA WAPELEKWA KUCHEZESHA MECHI YA SIMBA MISRI...ISHU IKO HIVI...