Home Habari za michezo BAADA YA KUPOTENA NA SIMBA…, MKUDE KUKAKABIDHIWA SHUGHULI ZA KANOUTE LEO..

BAADA YA KUPOTENA NA SIMBA…, MKUDE KUKAKABIDHIWA SHUGHULI ZA KANOUTE LEO..

Habari za Simba leo

Kiungo wa klabu ya Simba Jonas Mkude anatarajiwa kuvaa viatu vya kiungo wa shoka ndani ya klabu hiyo ambaye atakosekana katika mchezo wa leo jumamosi dhidi ya Raja Casablanca Sadio Kanoute.

Kiungo Sadio Knaoute atakosekana katika mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa siku ya leo jumamosi kutokana na adhabu ya kadi aliyoipata katika mchezo uliopita dhidi ya klabu ya Horoya, Hivo Kiungo Jonas Mkude anatarajiwa kuvaa viatu vya kiungo huyo wa kimataifa wa Mali.

Akizungumza na kituo kimoja cha Redio Afisa habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema kua kiungo Jonas Mkude atakuepo kwenye mchezo wa jumamosi dhidi ya Raja baada ya kukosekana katika mchezo dhidi ya Horoya, Huku akisisitiza kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji kwenye eneo la katikati anaetarajiwa kuvaa viatu vya Kanoute.

Kiungo Sadio Kanoute amekua mhimili mkubwa kwenye eneo la katikati la klabu ya Simba kwa msimu wa pili na pale anapokosekana klabu hiyo imekua ikitetereka kwa kiasi fulani, Kukosekana kwake siku ya leo ni pigo kubwa ndani ya klabu hiyo.

Kupitia Afisa habari Ahmed Ally pia alieleza kua kiungo Jonas Mkude yupo kambini kwenye timu hiyo na wenzake na kuzima tetesi zinazoeleza kua kiungo huyo yupo kwenye matatizo na klabu ya Simba na hayupo kambini, Lakini msemaji huyo aliweka wazi kua kiungo huyo aliedumu klabuni hapo kwa muda mrefu zaidi atakuepo katika mchezo wa leo.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA KUPEWA UKOCHA TAIFA STARS....NABI AANIKA MUSTAKABALI WAKE NA YANGA...