Home Yanga SC YANGA: MALENGO YETU YAPO PALEPALE

YANGA: MALENGO YETU YAPO PALEPALE

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa malengo yao makubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara yapo palepale licha ya kuwa kwenye mwendo wa kusuasua.

Kwenye mzunguko wa kwanza Yanga ilianza kwa kasi nzuri na ilicheza jumla ya mechi 19 bila kupoteza ila ilipocheza mechi tano ilibadili benchi la ufundi kwa kumfuta kazi Zlatko Krmpotic.

Krmpotic alishinda mechi nne na kuambulia sare moja ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa kwa sare ya kufungana bao 1-1 na alifutwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni matokeo mabovu.  

Mrithi wa mikoba yake, Cedric Kaze yeye aliongoza kwenye mechi 18, alishinda 10, sare 7 na kichapo moja akachimbishwa Machi 7 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo mbovu wa timu.

Mchezo wake wa mwisho ubao ulisoma, Polisi Tanzania 1-1 Yanga jambo lililowafanya mabosi wamfute kazi.

Ikiwa ipo nafasi ya kwanza imekuwa ikipata presha kubwa kutoka kwa watani zao wa jadi Simba ambao ni mabingwa watetezi, wapo nafasi ya pili na pointi zao ni 46 huku vinara wakiwa na pointi 50.

Mshindo Msola Mwenyekiti wa Yanga amesema:-“Malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara yapo palepale, kushindwa kupata matokeo kwenye mechi zilizopita haina maana kwamba tutashindwa kufikia malengo yetu.

“Tuliamua kufuta benchi la ufundi ili kuweza kutatua tatizo la matokeo mabaya hivyo bado kazi inaendelea na malengo hayabadiliki”.


SOMA NA HII  MZEE MPILI: TUNAIFUNGA SIMBA TENA KIGOMA, MANARA ANIPE MILIONI YANGU