Home Yanga SC MZEE MPILI: TUNAIFUNGA SIMBA TENA KIGOMA, MANARA ANIPE MILIONI YANGU

MZEE MPILI: TUNAIFUNGA SIMBA TENA KIGOMA, MANARA ANIPE MILIONI YANGU


 HAJI Omari Mpili, maarufu kama Mzee Mpili amesema kuwa hawezi kushindana na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kwa kuwa ni mtoto mdogo na lazima ataifunga tena Simba watakapokutana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Mzee Mpili amebainisha kuwa ushindi wao wa Julai 3 yeye alikuwa ni mchezaji namba moja kwa kuwa ana watu hivyo hana mashaka na mchezo wao kuelekea Julai 25 na amesisitiza kwamba lazima alipwe mkwanja ambao aliahidiwa na Manara ambao ni milioni moja.

“Mimi ninasema kwamba mchezo wetu ule pale taifa nilikuwa mchezaji namba moja na kuelekea kwenye mchezo wetu Kigoma nina amini kwamba nitaucheza na tutashinda.

“Siwezi kushindana na Manara, yeye ni mtoto mdogo haniwezi na mimi nina watu wakubwa kila mahali, sasa ninasema hivi kwa kuwa aliniahidi atanipa milioni moja ninaitaka.

“Yeye mwenyewe Manara alisema kuwa ohh Mzee Mpili ukitufunga sisi nitakupa milioni moja, basi sikumuomba mwenyewe amesema naitaka milioni moja yangu na ninasema kwamba Kigoma tunashinda tena,” amesema.

Katika mchezo wa Julai 3, Simba ilishuhudia dk 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-1 Yanga na bao pekee la ushindi lilifungwa na Zawad Mauya dk 12.

SOMA NA HII  MTEGO WA MAYELE YANGA SASA HADHARANI