Home Uncategorized SITA WATUSUA KWENYE SHINDANO LA CHOMOKA NA GARI JIPYA, WAOGELEA MINOTI

SITA WATUSUA KWENYE SHINDANO LA CHOMOKA NA GARI JIPYA, WAOGELEA MINOTI

DROO ya pili ya bahati nasibu ya Jishindie Gari na Championi na Spoti Xtra (maarufu kama promosheni ya Baba Lao ama Chomoka na Gari Mpya Toyota Fun Cargo) ilifanyika leo Jumanne, Aprili 21, 2020 katika ofisi za Global Group na kufanikiwa kupata washindi sita.

Hii inakuwa ni idadi kubwa ya washindi ukilinganisha na ile droo ya kwanza ambayo ilitoa washindi watatu kutoka katika mikoa tofauti. 


Washindi wote sita ambao wametoka katika mikoa mbalimbali watazawadia fedha taslimu shilingi 50,000 kila mmoja pamoja na tisheti mpya.

Droo hiyo ambayo imechezeshwa na shabiki wa Simba Sc, Humphrey Msungu, imerushwa na Televisheni namba moja ya mtandaoni nchini, Global TV Online, ili kuweka wazi kwa washiriki wengine na Watanzania wote kwa ujumla na kuondoa ile dhana ya kwamba washindi huenda wanatengenezwa.


Mkuu wa Idara ya Masoko wa Global Publishers ambao ndiyo waandaaji wa promosheni hiyo kupitia magazeti ya michezo, Championi na Spoti Xtra, Antony Adam aliwataja washindi hao kuwa ni Yassin Seleman wa Kibaha Pwani, Samson Kabuje wa Mbeya, Aloyce Mdolwa wa Mwanza, Hassan Khatau wa Dar es salaam, Mwinjuma Ngayama wa Tanga na Yuda Mrema wa Moshi.

Adam alitoa sababu ya kubadilisha zawadi ya kutoa simu katika droo ya kwanza na kutoa fedha, akisema kuwa ni kujali hali za wananchi kutokana na janga la Corona ambapo watu wengi hawana fedha za kujikimu kutokana uchumi kuyumba.


 “Tumeamua kubadilisha zawadi kidogo safari hii kutokana na ishu ya Corona, watu wengi ni kama hawana fedha kutokana na uchumi kutokuwa sawa kutokana na Corona, kwahiyo tukitoa shilingi 50,000, itawawasaidia katika kununua mahitaji mbalimbali ya nyumbani katika kipindi hiki. 

“Kwahiyo kila mshindi atatumiwa fedha yake kesho Jumatano, ambapo mbali na fedha tutawapatia pia na zawadi za tisheti kama nyongeza,” amesema Anthony.


Bahati nasibu hii, itatoa zawadi ya gari mpya ana ya Toyota FunCargo, hicho ndiyo kitu pekee ambacho unatakiwa kukizingatia, hizi simu na zawadi nyingine kama fedha na tisheti ambazo zitakuwa zinatoka kwenye droo ndogo kabla ya ile kubwa kufanyika mwezi ujao.

SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI WA LIPULI ANAPIGA TIZI MARA MBILI KWA SIKU