Home news KAMBI YA SIMBA MOROCCO IMEZUA JAMBO HILI

KAMBI YA SIMBA MOROCCO IMEZUA JAMBO HILI


 BENCHI la ufundi la Simba limeweka wazi kuwa kambi yao ya nchini Morocco ilikuwa nzuri kutokana na kila mmoja kuifurahia kambi hiyo na jambo kubwa ambalo limeweza kuonekana ni uwezo wa wachezaji pamoja na ushirikiano kiujumla.


Mabingwa hao watetezi kwa msimu wa 2021/22 waliweza kucheza mechi mbili za kirafiki ilikuwa dhidi ya FAR Rabat na waliweza kufungana mabao 2-2 na mchezo dhidi ya Olympique Club de Khouribga na walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.


Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa walikuwa katika nzuri ya maandalizi ya msimu mpya jambo ambalo ni furaha kwao.


“Kambi yetu ya Morocco ilikuwa ni ya furaha kwa kila mmoja na tunashukuru Mungu tumeweza kurudi salama, ilikuwa ni jambo zuri kwa kila mmoja na tumeweza kupata kitu kizuri kwa ajili ya msimu mpya hivyo mipango mingine itajulikana.


“Kuwa pamoja kwa muda mrefu ni moja ya mambo ambayo yanatupa nafasi ya kujua mwanzo wa msimu tutaanzaje na kwa namna ligi ambavyo ilivyo inaonyesha wazi kabisa ushindani utakuwa mkubwa nasi tupo tayari,” amesema Matola.

Kwa sasa kikosi cha Simba kimeweka kambi Arusha na watakuwa na mechi za kirafiki kwa ajili ya kujiweka sawa.

Pia watakuwa na mechi za kirafiki ambazo zitakuwa maalumu kwa ajili ya kuelekea Simba Day kwa ajili ya utambulisho wa wachezaji na uzi mpya.

Ni Septemba 19 Simba wanatarajia kufanya tamasha hilo linasubiriwa kwa shauku na mashabiki pamoja na wadau wa soka.

Miongoni mwa nyota ambao walikuwa nchini Morocco na wamejiunga pia na kambi ya Arusha ni pamoja na Pascal Wawa, Jonas Mkude, Ibrahim Ajibu na Chris Mugalu.

SOMA NA HII  ILI KUWAMALIZA KABISA WANIGERIA...MAYELE AWEKEWA MIL 300 CASH MEZANI....