Home news MTIBWA SUGAR KUZIPELEKA SIMBA V YANGA MANUNGU

MTIBWA SUGAR KUZIPELEKA SIMBA V YANGA MANUNGU


 MTIBWA Sugar imesema kwamba, ipo kwenye hatua nzuri ya kuufanyia marekebisho uwanja wao wa Manungu ili waweze kuutumia kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya timu zote ikiwemo Simba na Yanga.

Uwanja huo wa nyumbani wa Mtibwa, ulifungiwa msimu uliopita na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutokana na kutokidhi vigezo na kuifanya timu hiyo kubadilisha uwanja kwa kuutumia Uwanja wa Jamhuri.

Msimu huu, Mtibwa imeshindwa pia kuutumia Uwanja wa Jamhuri, ambapo katika mechi zake mbili za kwanza za Ligi Kuu Bara, imetumia Uwanja wa Mabatini uliopo Pwani na Uhuru, Dar.

Hii pia imetokana na ule Uwanja wa Jamuhri,Moro kutokidhi vigezo vya kuchezea mechi za ligi.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, alisema: โ€œKuhusu uwanja wetu wa Manungu uliopo Turiani, tumeshakamilisha marekebisho ya eneo la kuchezea na tayari tumeweka uzio.

โ€œKinachoendelea kwa sasa ni ujenzi wa ukuta ambao utachukua wiki nne kukamilika, hivyo tunatarajia mechi za Simba na Yanga tutacheza kwenye uwanja wetu.โ€

Uwanja huo ni moja ya viwanja ambavyo vilikuwa vikiipa matokeo Mtibwa Sugar inayonolewa kwa sasa na Kocha Mkuu, Joseph Omog.

SOMA NA HII  SIMBA HALI SI SHWARI LIGI KUU...... NAMUNGO WAFANYA UKATILI WA KULAZIMISHANA