Home Simba SC CLATOUS CHAMA APEWA UFALME NDANI YA SIMBA YA GOMES

CLATOUS CHAMA APEWA UFALME NDANI YA SIMBA YA GOMES


 KUHUSIKA kwenye mabao 15 ndani ya Simba kwa Clatous Chama kati ya mabao 42 kumempa ufalme nyota huyo na kudhihirisha kuwa asipokuwa sawa ama kutokuwepo kikosini mambo huwa magumu.


Ikumbukwe kuwa kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 Simba imepoteza mechi mbili, ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting na kwenye mechi hizo Chama hakuwepo.

Akiwa amefunga jumla ya mabao sita na pasi tisa ni kinara wa kutengeneza nafasi za mabao ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes.

Pia na kwenye ligi kiujumla yeye ni namba moja kwa kutengeneza pasi za mwisho huku mfunaia nyavu namba moja akiwa ni meddie Kagere wa Simba mwenye mabao 9.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ikiwa Chama hatakuwa fiti ndani ya kikosi hicho huwa inakuwa ngumu kupata ushindi.

“Ikiwa Chama,(Clatous) hatakuwa fiti kwenye mchezo basi huwa inakuwa ngumu kupata ushindi lakini akiwa fiti kwa asilimia walau 75 basi hakuna anayeshinda ila akifika asilimia 100 hata Barcelona anapigwa,” amesema.

SOMA NA HII  KUHUSU ALLY SALIM 'KUIKAZIA' YANGA JANA...KUMBE SIRI YA NYUMA YA PAZIA NI HII....