Home Ligi Kuu KMC YATENGA DAKIKA 270 ZA KUSAKA USHINDI

KMC YATENGA DAKIKA 270 ZA KUSAKA USHINDI


 UONGOZI wa KMC umesema kuwa una mechi tatu za kazi ambazo ni dakika 270 za kusaka ushindi ndani ya uwanja.

Mechi hizo ni zile za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho ambalo bingwa mtetezi wa taji hilo ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes.

Kete ya kwanza kwa KMC itakuwa ni Februari 26, Uwanja wa Uhuru ambapo itakuwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora.


Baada ya kumaliza dakika zake 90 hapo itakuwa na kazi nyingine Machi 4 ni Uwanja wa sheikh Amri Abeid mbele ya Polisi Tanzania na kumaliza na Coastal Union, 7 hizi mbili zitakuwa za ligi.

 Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa tayari kikosi kimeanza maandalizi kwa ajili ya mechi zao zote zinazowakabili.

“Tumeanza maandalizi kwa ajili ya mechi zetu tatu zilizopo mbele yetu na jambo ambalo tunahitaji ni ushindi ndani ya uwanja bila kujali tunakutana na timu ipi, mashabiki watupe sapoti.

“Kikubwa ambacho huwa tunatazama ni maandalizi ya mechi pamoja na kuwaheshimu wapinzani wetu ambao tunakutana nao hakuna timu ndogo ndani ya uwanja zote ni sawa,” amesema.

KMC ipo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 21 msimu wa 2020/21.

SOMA NA HII  RUVU SHOOTING YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA