MKONGWE katika gemu la Bongo Fleva, Dully Sykes, amesema kuwa ngoma yake mpya ya Nikomeshe hajaitunga yeye bali ni ubunifu tu ameufanya kwenye kazi yake ya sanaa.
Nyota huyo wa muziki wa vijana, amesema amekuwa karibu na Harmonize kwa ajili ya kufanya muziki wa kibiashara.
“Katika wimbo wangu mpya na Harmonize wa Nikomeshe, ule kwanza sikutunga mimi, nilimwambia Harmonize anitengenezee wimbo wote, mimi nilienda kuimba tu. Kwa hiyo ni ubunifu tu.
“Ukiona Harmonize ameweka katika ukurasa wake wa Youtube ile ni kazi, basi ujue ni yetu wote. Vidole viko vitano, unafikiri ukikata vinne kimoja kitakuwa na kazi gani?,” amesema Dully.