Home Habari za michezo HUU HAPA UKWELI KUHUSU WACHEZAJI WA SIMBA NA MCHEZO WA SIMBA DAY….

HUU HAPA UKWELI KUHUSU WACHEZAJI WA SIMBA NA MCHEZO WA SIMBA DAY….

Kikosi cha Simba Msimu huu 23/24

Wachezaji wa Simba waliotambulishwa katika Simba Day Wapo 30 ila Waliokuwepo katika sehemu ya mchezo wa Jana dhidi ya Power Dynamos ni 23 tu.

Katika Mchezo kuna Taratibu zake kwa jana katika Wachezaji 11 wataoanza ndani utaweza kufanya Mabadiliko mkupuo Mitatu na idadi ya mwisho ni Wachezaji 7 tu na hii ilitokana na Timu ya Power Dynamos kuja Tanzania na Idadi ya jumla ya Wachezaji 18 hivyo wakianza 11 nje wanakuwepo 7 kwa maana huwezi kuendelea kubadili wakati timu nyingine haiwezi kubadili zaidi.

Simba walikuwa na wachezaji ila walipaswa ndani kuwa 11 na nje 12 lakini wakitakiwa kufanya Mabadiliko 7 jumla 18 na Wachezaji 5 waliobaki katika mchezo ila hawawezi kuingia kucheza.

Ukiangalia Katika Kikosi kizima Wachezaji waliocheza Muda wote wa dakika 90 ni Wanne tu Kipa Ally Salim, Tshabalala, Kapombe na Che Malone wengine wote 7 waliweza kubadilishana wa walioko nje kwa namba zinazoendana kwa nafasi husika.

Simba imesajili Wachezaji Wapya 10 kati ya wale waliotambulishwa kati yake Watano wa Tanzania na Watano wa nje, katika Wachezaji wote 10 wapya walikuwepo sehemu ya mchezo wa jana ni 7 ambao wa nje wote 5 na wa ndani 2 wasiokuwepo ni Watatu nao ni Chilunda, Duchu na kipa Hussein Abel.

Katika Wachezaji 7 wapya waliokuwepo sehemu ya mchezo wa jana Walioanza mchezo ni Wawili Onana na Che Malone halafu Wengine Watano wote Waliingia katika mabadiliko 7 yaliyofanyika na ambao nafasi mbili zilikuwa na zamani nao ni Baleke na Kapten Bocco hawa walicheza katikati wakati pembeni winga zote walikuwepo Luis Miquissone na Kramo kati nyuma Ngoma hii ikawa safu nzima ya mbele mpya nje ya ila ya kwanza ilikuwa pembeni Onana na Kibu kati Chama na Saidoo nyuma yao wakiwa Kanoute na Mzamiru.

Wachezaji wote walikuwepo sehemu ya mchezo wale 23 ila hawajaweza kucheza Wale Watano ni Wachezaji wa zamani Waliokuwepo Phiri, Kennedy, Mwanuke, Mwenda na Kipa Ferouz unaweza kujiuliza Kwanini hawa wahaweza kucheza jana ni kutoana na makubaliano ya Utaratibu wa mchezo katika idadi ya mabadiliko ya wachezaji ila pia unaweza jiuliza hata fulani kweli hajaweza kucheza katika hao wengine ni kuwa katika Mabadiliko 7 yakufanya watano ni wapya lazima wacheze wa zamani walioingia ni Baleke na Bocco Je unawezaje kumuacha mtu alimaliza msimu vizuri nje na Je unawezaje kumuacha Legend na siku yake ya kuzaliwa jana na ndio Kapten Mkuu tuwe na subra Kikosi ni kipana sana na kinataka Technical Bench kutulia sana kwa Makocha maana Ukiangalia Ndani Mtu nje mtu na wa nje akiingia nje kuna mtu nae anasubiria hii ndio Simba ambayo ilitakiwa kuwa Vyuma pande zote muda wote hata ikitokea majeruhi hakuna matatizo.

Kilichobaki ni kupata Muda kwa kikosi kuungana na kutengeneza Chemistry nzuri sana na muda tutaona maana Tunaanza na Ligi kwanza mechi za CAF ni baadae hapa tunaambiwa HATUJAMALIZAAAA.

@MtiMkavu“`

SOMA NA HII  KIFAA KIPYA YANGA CHAANZA NA MKWARA WA KUFA MTU...AJITOFAUTISHA NA WENZAKE...