Home Habari za michezo GAMONDI AMKINGIA KIFUA HAFIZ KONKANI, ISHU IKO HIVI

GAMONDI AMKINGIA KIFUA HAFIZ KONKANI, ISHU IKO HIVI

Habari za Yanga

Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi amesema kuwa anafurahi kuona mshambuliaji wake mpya, Hafiz Konkoni anaanza kufunga mabao ndani ya timu hiyo huku akiamini makubwa kutoka kwa mchezaji huyo.

Konkoni ni ingizo jipya ndani ya Young Africans akisajiliwa kutoka klabu ya Bechem United ya Ghana ambapo tayari ameanza kufungua akaunti ya mabao ndani ya Young Africans baada ya kufunga bao katika mchezo wa ligi dhidi

Akizungumza jijini Dar es salaam, Gamondi amesema kuwa kitendo cha kufunga bao kwa Konkoni kimemfurahisha kwa kuwa kitampa hali nzuri ya kuendelea kujiamini kwa kumpunguzia presha ambayo pengine angeendelea kuwa nayo ya kucheza bila kupata bao jambo ambalo kwake anazidi kupata mnatumaini makubwa.

“Kwa mchezaji ambaye anacheza katika eneo la ushambuliaji kitendo cha kucheza michezo mitatu bila kufunga bao, ni jambo ambalo humpa mawazo mshambuliaji yeyote, kwa watu wanaocheza nafasi za ushambuliaji furaha yao kubwa ni kuweza kuhakikisha kuwa wanafunga mabao mengine hayo ni baadae.

Ndio maana hata kwa upande wangu nimefurahi kumuona mshambuliaji wangu akifunga bao kwa kuwa naamini itamuongezea nguvu ya kupambana na kujiamini kwani itamuondolea ile presha ambayo angeweza kukutana nayo au kumkumba pale ambapo angeshindwa kufunga katika michezo ijayo. Mimi binafsi naamini kuna makubwa kutoka kwake”

SOMA NA HII  MCHEZO WA SIMBA V POLISI TANZANIA WAPELEKWA MBELE