Home Habari za michezo SIMBA WAIFANANISHA AL AHLY NA ZAMALEK

SIMBA WAIFANANISHA AL AHLY NA ZAMALEK

Habari za Simba

Uongozi wa Klabu ya Simba imesema kuwa unatambua mchezo wao wa nusu fainali ya African Football League dhidi ya Al Ahly ni mgumu ndani na nje ya uwanja hivyo wamejidhatititi kuhakikisha wanapata matokeo chanya na kusonga mbele.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally wakati akizungumza na wanahabari nchini humo kuelekea mchezo huo utakaopigwa leo Oktoba 24, 2023 nchini Misri baada ya ule wa kwanza kumalizika kwa sare ya bao 2-2 katika Dimba la Mkapa.

“Tunakwenda kucheza kwenye moja ya viwanja vikubwa barani Afrika na wenye heshima kubwa. Uwanja wa Cairo International ni moja ya viwanja vigumu kuvicheza, ndiyo uwanja wa nyumbani wa Al Ahly na Zamalek na ndiyo uwanja wa Taifa wa Misri. Ahly wameuzoea kwa sababu wanautumia kila siku.

“Ni mechi ngumu lakini Simba tunahitaji kuandika historia mpya baada ya miaka 20 ambapo tulimtoa Zamalek mwaka 2003 kwenye mashindano. Hivyo tunataka kuwatoa wapinzani wa Zamalek katika uwanja huo huo.

“Tunajua ugumu wa mechi kuanzia nje mpaka ndani ya uwanja, mashabiki wao watajaa, watashangilia, wataimba mwanzo mwisho kwa nguvu, lakini sisi tutapambana na vikwazo vyote vya ndani na nje ya uwanja ili wachezaji wetu wajikitike kwenye mechi uwanjani tu,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  HIKI HAPA NDIO KINACHOENDA KUTOKEA KWA YANGA NA GAMONDI WAKE