Home Azam FC AZAM FC YARUDISHA SHUKRANI KWA MASHABIKI, MAPOKEZI YAO ACHA KABISA

AZAM FC YARUDISHA SHUKRANI KWA MASHABIKI, MAPOKEZI YAO ACHA KABISA


 UONGOZI wa Azam FC umewashukuru mashabiki wa timu hiyo ambao walijitokeza kuwapokea baada ya kuwasili Songea jana, Juni 23.

Kikosi hicho kwa sasa kipo Songea na jana kilifanya mazoezi mepesi ili kurejea kwenye ubora wao na leo pia wataendelea na mazoezi.

 Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wamefurahishwa na mapokezi ambayo wameyapata kwa kuwa yalikuwa ni mazuri.

“Mapokezi ambayo yamefanywa na mashabiki wetu wa Songea ni makubwa na kila mmoja ameweza kuona namna gani tunapendwa kila kona.

“Ukweli ni kwamba tunawashukuru mashabiki kwa namna ambavyo wametupokea na tunaomba waendelee na sapoti yao bila kuchoka,” amesema.

Juni 26, Azam FC itakuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali itakuwa dhidi ya Simba.

Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Majimaji ambapo mshindi kwenye mchezo huo atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Biashara United na Yanga.

SOMA NA HII  WAKATI WAKICHEKA NA USAJILI WA FEI TOTO...RUNGU LA CAF KUWASHUKIA AZAM ENDAPO HILI HALITAFANYIKA...