Home Yanga SC YANGA WATAJA SABABU ZA KUCHUKUA UBINGWA WA SIMBA

YANGA WATAJA SABABU ZA KUCHUKUA UBINGWA WA SIMBA


HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa bado wana nafasi ya kutwaa ubingwa kwa kuwa kikosi chao kinazidi kuimarika kila leo.

Kwenye mataji yote mawili ikiwa ni la ligi pamoja na lile la Kombe la Shirikisho mabingwa watetezi ni Simba ambapo wametinga hatua ya fainali kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC huku Yanga wakitinga hatua ya fainali kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United.


Yanga ipo katika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, huku ikiwa na pointi 67 ikiongozwa na kinara wa Simba wenye pointi 73.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Bumbuli alisema kuwa kila kitu kipo katika utaratibu wake katika suala la maandalizi, kwa hiyo wamejipanga kuchukua ubingwa wa FA.

 

“Maandalizi yanaendelea vizuri kama kawaida, niseme tu kwamba tumejipanga kuchukua ubingwa katika pande zote.

 

“Kikosi chetu kinazidi kuimarika kila siku na sitaki kuongea sana, lakini mtajionea wenyewe kinachoenda kutokea, lazima tuchukue ubingwa,” alisema Bumbuli.


Julai 25, mwaka huu, Yanga na Simba zinatarajiwa kupambana katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam maarufu FA.


Pia kwenye ligi, Julai 3 wanatarajiwa kukutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao unatarajiwa kuwa na  ushindani mkubwa.

SOMA NA HII  SAKATA LA MAYELE KUSEPA JANGWANI...LACHUKUA SURA MPYA...SENZO AIBUKA NA HOJA TATA.."AKIUZWA NASEPA YANGA"...