Home Habari za michezo MASHABIKI WA YANGA HAPO KIGALI SIO POA

MASHABIKI WA YANGA HAPO KIGALI SIO POA

YANGAKULITETEA TAJI LAO...TUMEWAACHA POINTI NYINGI WANAOTUFATA...TUNAPAMBANIA MATAJI YOTE

Licha ya kusalia kwa siku chache kabla ya Young Africans kuvaana na Al Merrikh ya Sudan kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, tayari klabu hiyo imeshakuwa gumzo nchini Rwanda ambapo utapigwa mchezo huo huku baadhi ya nyota wake wakiwa wameiteka nchi hiyo kwa kutajwa sana na mashabiki.

Miongoni mwa majina ambayo yanazungumzwa zaidi kwa mastaa wa Young Africans ni kiungo mshambuliaji Maxi Mpia Nzengeli na Pacome Zouzoua ambao licha ya kusajiliwa msimu huu wamekuwa moto kutokana na uwezo waliounyesha klabuni hapo.

Chanzo kutoka nchini Rwanda kimeeleza kuwa nyota hao wawili sambamba na wengine wa tỉmu hiyo wamekuwa wakitajwa kwa wingi na mashabiki wamejiandaa vilivyo kuwatazama siku ya mechi hiyo.

“Unajua tangu msimu unaanza mashabiki hapa nchini wamekuwa wakiifuatilia Young Africans kwa ukaribu na viwango vya mastaa wa timu hiyo wamekuwa wakivijua, ndiyo maana wanawazungumzia sana.

“Nadhani siku ya mechi hiyo kutakuwa na idadi kubwa ya mashabiki ambao watajitokeza uwanjani kwa kuwa watataka kuwaona wenyewe namna wanavyocheza na viwango vyao kama wanavyowaona sasa kwenye runinga,” kimesemna chanzo hicho.

Katika hatua nyingine Young Africans wamepewa siri za wapinzani wao Al Merrikh na nyota wao wa zamani, Patrick Sibomana ambaye amesema kwa namna ambavyo amewaona Wasudani hao wakicheza basi Wananchi wana uhakika wa kupata ushindi.

“Nimewatazama Al Merrikh wakiwa huku Rwanda ambapo walicheza mchezo wao wa kimataifa, kwa ambavyo Young Africans nimewaona wanavyocheza naamini wanayo nafasi nzuri ya kufanya vyema mbele yao.

“Kwa mashabiki, wachezaji na viongozi wote wa Young Africans niwakaribishe sana Rwanda, huku ni nyumbani kwao na niwahakikishie tu kwamba wasijisikie uvivu kuja na mimi nawatakia safari njema ya kuja huku,” amesema mchezaji huyo.

SOMA NA HII  MZIMU WA MAYELE WAENDELEA KUSAKAMA YANGA, KUMPATA MRITHI WAKE MAJANGA, MPOLE AHUSISHWA