Home Habari za michezo BAADA YA KUUWASHA AKIWA NA STARS AFCON…..’BACCA’ HUYOOOO MAJUUU…HII NI LAZIMA…

BAADA YA KUUWASHA AKIWA NA STARS AFCON…..’BACCA’ HUYOOOO MAJUUU…HII NI LAZIMA…

Habari za Michezo leo

Wakati kikosi cha Taifa Stars kikijipanga kuanza safari ya kurejea nchini Tanzania, beki wa timu hiyo Ibrahim Hamad ‘Bacca’ ndio jina linalowapasua maskauti wengi kwenye kambi ya Stars.

Mara baada ya mchezo wa Stars na DR Congo kumalizika mmoja wa makocha waliopo kwenye Kambi ya Stars amesema maskauti watatu tofauti wametinga kambini kwao wakiulizia taarifa zaidi za beki huyo.

Kwenye maswali ambayo maskauti hao wamekuwa wakiuliza ni kutaka kujua zaidi juu ya klabu ambayo anaitumikia endapo viongozi wao wapo nchini Ivory Coast.

Mbali na swali hilo pia imetaka kujua kama beki huyo aliwahi kwenda kujaribu soka nje ya kucheza Tanzania huku wakimsifia kwa ubora ambao ameonyesha.

“Wamemsifia sana Bacca, wako maskauti watatu lakini wawili hao ndio kama wamekuwa wakimfuatilia zaidi wakipishana kutafuta taarifa zake zaidi,”amesema kocha huyo ambaye hakutaka kutajwa kwa jina lake.

“Kwa kiwango ambacho amekionyesha sishangai kutafutwa hivi lakini pia najiandaa kusikia lolote baada ya hizi mechi hasa kutoka klabuni kwake kama Hawa watu watakuwa wana muendelezo wa kuifikia klabu yake.

“Tanzania ili ifanye vizuri tunahitaji sana watu kama Bacca waonyeshe uwezo na watoke kwenda kuonyesha uwezo wao zaidi.

Kwenye mechi tatu ambazo Stars imecheza hatua ya makundi Bacca amekuwa akionekana kwenye takwimu nyingi za ubora na hata vikosi vya bora vya mechi za siku kutokana na ubora mkubwa alipokuwa anauonyesha kwenye safu ya ulinzi ya timu yake.

SOMA NA HII  KOCHA MSOMALI WA AZAM FC APIGA MKWARA YANGA..AFUNGUKA 'ATAKAVYOWATOBOLEA MTUMBWI'...