Home Uncategorized GWAMBINA WATUMIA DAKIKA 90 KUSOMA MBINU ZA SIMBA

GWAMBINA WATUMIA DAKIKA 90 KUSOMA MBINU ZA SIMBA


 JACOB Massawe, nahodha wa Gwambina amesema kuwa walitumia dakika 90, Septemba 20 kuitazama mechi ya wapinzani wao Simba wakiwa kambini jambo linalowapa matumaini ya kupata matokeo mazuri kwa kuwa wametambua mbinu za wapinzani wao.

Gwambina ambayo inashiriki Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza msimu huu wa 2020/21 baada ya kupanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza ina kibarua cha kumenyana na Simba, Septemba 26, Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na Championi Jumatano, Massawe alisema kuwa wachezaji wote wakiwa kambini Kibaha walikaa chini na kutumia dakika 90 kutazama mechi hiyo ambapo Simba ilishinda mabao 4-0.


“Kwa sasa tupo Kibaha tukijiandaa na mchezo wetu dhidi ya Simba, Septemba 20 tulikaa chini pamoja na wachezaji wote kutazama namna wapinzani wetu wanavyocheza,tumewaona na tunawaheshimu kwani ni timu bora, ila tutapambana kupata matokeo chanya,” alisema.

Gwambina itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Pwani na ni mchezo wa kwanza kukutana na Simba kwenye ligi.

SOMA NA HII  NYOTA NGORONGORO HEROES KUWAKOSA SAUDI ARABIA