Home news MAKOCHA YANGA WAVAMIA MECHI YA SIMBA vs NAMUNGO…NABI AJIFUNIKA NA KOFIA NYEUSI..

MAKOCHA YANGA WAVAMIA MECHI YA SIMBA vs NAMUNGO…NABI AJIFUNIKA NA KOFIA NYEUSI..


KOCHA wa Yanga, Nabi Nesreddine ni miongoni mwa watazamaji wa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Namungo.

Kocha huyo ambaye ameiongoza Yanga kuibuka na ushindi kwenye mchezo mitano mfululizo ya Ligi Kuu Bara, anaonekana kuwa mtulivu huku akiwa ameshika tama ishara ya kuufuatilia mchezo huo kwa umakini mkubwa.

Nabi aliyevalia kofia nyeusi, anaonekana kuwasoma Namungo ambao baada ya wiki ya Kimataifa atakuwa na mchezo dhidi yao Novemba  20 huko kusini mwa Tanzania.

Hivyo hii ni fursa kwa Mtunisia huyo kuona namna gani mbavyo  atawaandaa vijana wake kwa ajili ya mchezo huo.

Ikumbukwe kuwa mara baada ya Yanga kucheza dhidi ya Namungo watarejea jijini Dar es Salaam kucheza dhidi ya Mbeya Kwanza kabla ya mchezo wa watani wa jadi, Desemba 12.

Nabi hayupo peke yake uwanjani hapa yupo na kocha msaidizi Cedric Kaze, meneja wa Yanga, Hafidh Saleh  licha ya kuwa wamekaa sehemu mbili tofauti mmoja, VIP A na mwingine B.

SOMA NA HII  BAADA YA KUIONA SIMBA INAVYOCHEZA...KAMUSOKO AIBUKA ..ATOA TAHADHARI MECHI NA WAZAMBIA...