Home news MRWANDA AFICHUA KILICHO NYUMA YA UBOVU WA SIMBA..AWATAJA WACHEZAJI NA NAMNA WALIVYOTUMIKA….

MRWANDA AFICHUA KILICHO NYUMA YA UBOVU WA SIMBA..AWATAJA WACHEZAJI NA NAMNA WALIVYOTUMIKA….


STAA wa zamani wa Simba, Danny Mrwanda ametamka kuwa pamoja na watu wengi kuibeza timu hiyo ana imani nayo msimu huu.

Katika mechi nne Simba ina mabao mawili iliyofunga dhidi ya Dodoma Jiji (Meddie Kagere) na Polisi Tanzania (Larry Bwalya -penati), ligi iliyoisha walikuwa na manne.

Simba ilivyoanza katika mechi nne msimu ulioisha ilishinda dhidi ya Ihefu (mabao 2-1), sare na Mtibwa Sugar (1-1), ilifungwa na Ruvu na Prisons, jambo ambalo wadau wameona kuna kitu kinatakiwa kifanyike ili ichangamke.

Mrwanda ambaye kwa sasa yupo Ken Gold, alisema bado ana imani na Simba kufanya vizuri msimu huu alichoshauri wachezaji wasahau mechi waliyofungwa ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kueleleza nguvu mbele yao.

“Pia wachezaji walitumika sana. Kuna wakati mwingine miili inakuwa imechoka, naamini wakikaa sawa watafunga tu mechi zilizopo mbele yao,” alisema.

Beki wa kati wa Biashara United, Abdulmajid Mangalu alisema tayari wamecheza na Simba hajaona ubaya wake isipokuwa wanatakiwa kutulia na kucheza kwa kujiamini.

Kocha Ulimboka Mwakingwe alisema bado anaiona nafasi ya Simba kufunga mabao mengi msimu huu. “Ngoja hao kina Kibu Denis, Bocco, Kagere na Mugalu wafungulie kufunga mabao. Upepo utabadilika na yataanza kuongelewa mengine,” alisema.

SOMA NA HII  MERIDIANBET WAINGIA LIGI KUU..., WAMWAGA PESA KWA KMC....!