Home Habari za michezo BARCELONA WAZIDI KUFULIA KIUCHUMI…MASTAA WADAI MALIMBIKIZO YA MISHAHARA …MCHEZAJI MADRID AWANANGA…

BARCELONA WAZIDI KUFULIA KIUCHUMI…MASTAA WADAI MALIMBIKIZO YA MISHAHARA …MCHEZAJI MADRID AWANANGA…


Klabu ya Barcelona imeripotiwa kudaiwa Euro milioni 102 za mishahara ya Manahodha wake wawili Gerard Pique na Sergio Busquets.

Tetesi zinasema Pique alikuwa tayari kukatwa mshahara , lakini pamoja na wiki kadhaa za majadiliano hadi sasa bado hawajafikia makubaliano.

Matatizo ya kifedha yanayoiandama klabu hiyo sio jambo geni na yamekuwa yakiathiri mambo kadhaa ikiwemo udumishaji na uhamisho wa wachezaji.

Hadi sasa Barca ina madeni yanayosemekana kufikia zaidi ya euro bilioni 1.

Mchezaji wa zamani wa Real Madrid Rafael van der Vaart aliongea kwa hisia akisema;

“mnawezaje kununua wachezaji wakati hamna pesa? hii ni fedheha, na Rais Laporta ambaye anaendelea kucheka kila sehemu huku akijigamba na akijiona yeye ni mfalme, lakini nadhani ni mjinga kiasi fulani.”

SOMA NA HII  FT: POLISI TZ 1-3 SIMBA SC ....PHIRI AMSAIDIA BOCCO KUMJIBU MAYELE..