Home Uncategorized LA LIGA, M-Bet, KUWAPIGA MSASA MAKOCHA

LA LIGA, M-Bet, KUWAPIGA MSASA MAKOCHA

 

KAMPUNI ya michezo ya kubahatisha ya M-Mbet na waendeshaji wa ligi ya Hispania, La Liga San Tander wameingia makubaliano ya kuendeleza vipaji nchini Tanzania.

Kampuni hizo mbili zimesaini mkataba wa miaka mitatu ambapo mbali ya kuendesha mafunzo ya soka kwa vijana, pia watafanya mafunzo kwa makocha na waamuzi kwa kutumia wataalam wa La Liga.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba, Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi amesema kuwa timu wanaoyoidhamini, KMC ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, nayo itafaidika na makubaliano hayo ambayo lengo lake kubwa ni kuendeleza mpira wa miguu nchini.

Mushi amesema kuwa safari ya M-bet ya kukuza soka la ndani ya nchi ilianza miaka miwili iliyopita na sasa wameamua kutanua wigo kwa kwenda kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.

“Lengo hapa ni kuwapa faida wateja wetu ambao ndiyo nguzo pekee katika maendeleo ya kampuni yetu, mara baada ya ligi ya Hispania mipaka kufunguliwa, wateja wetu wataweza kubashiri na washindi watakwenda kuangalia ligi hiyo ya Hispania,” amesema Mushi.

Amesema kuwa ushirikiano huo wataweza kukuza vipaji na kutimiza ndoto za vijana ambao ndiyo nguzo kubwa ya maendeleo ya soka nchini,” amesema Mushi.

Mwakilishi wa La Liga San Tander wa Tanzania, Alvaro Paya amesema kuwa wamefurahi kuingia makubaliano na M-Bet na kuwa washirika wa pili baada ya Klabu ya Yanga kuingia nayo makubaliano.

Paya amesema kuwa lengo la La Liga ni kuhakikisha mpira wa Tanzania unasonga mbele kwani wamegundua kuna vijana wengi wenye nia ya kuendeleza vipaji vyao, lakini wanakosa njia ya kufikia kwenye ndoto zao.

SOMA NA HII  FERNANDES ATAKATA UNITED IKIICHAPA MABAO 3-0 BRIGHTON