Home Uncategorized MCHEKA NYAVU WA MBAO FC AWAOMBA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA

MCHEKA NYAVU WA MBAO FC AWAOMBA WATANZANIA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA


WAZIRI Jr mshambuliaji anayekipiga ndani ya Mbao FC amesema kuwa kwa sasa anajifua ili kulinda kipaji chake pamoja na kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona.

Jr ana tuzo ya mchezaji bora Ligi Kuu Bara mwezi Februari timu yake ipo nafasi ya 19 baada ya kucheza mechi 29 na kibindoni ina pointi 23.

Nyota huyo amesema:”Hili ni janga la dunia nzima ni muhimu kuchukua tahadhari hicho ndicho ninachokifanya na pia ninalinda kipaji changu kwa kufanya mazoezi.

“Mashabiki na watanzania kiujumla ni wakati wetu wa kuendelea kufuata taratibu ambazo zinatolewa na Serikali kwani afya ni muhimu kwa ajili ya maendeleo yetu,”.

Kwenye Ligi Kuu Bara, nyota huyo ametupia mabao saba na pasi mbili za mabao huku Mbao ikiwa imefunga mabao 19.

SOMA NA HII  WALIOTOKA YANGA WAWA PASUA KICHWA AZAM FC