Home Uncategorized TEGETE AWAOMBA WATANZANIA KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI

TEGETE AWAOMBA WATANZANIA KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI

JERSON Tegete nyota wa zamani wa Yanga anayekipiga ndani ya Klabu ya Alliance amesema kuwa ni muhimu kwa kila mmoja kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya Corona ili awe salama.

Alliance yenye maskani yake mkoani Mwanza ipo nafasi ya 18 kwenye msimamo imecheza mechi 29 kibindoni imekusanya pointi 29.

Tegete amesema:”Ikiwa hauna shughuli ya lazima ya kufanya ikiwa ni kusafiri ni busara kubaki nyumbani na kuchukua tahadhari ili uwe salama.

“Janga hili ni kubwa na ni letu sote hivyo itapendeza kila mmoja akiwa anapambana kwa juhudi kushinda hili kwani mambo sio shwari, nami nachukua pia tahadhari,” amesema.

SOMA NA HII  SAMATTA AWEKA REKODI MOJA MATATA SANA, KAMTUNGUA GUARDIOLA HANA HAMU NAYE