Home Uncategorized SAMATTA AWEKA REKODI MOJA MATATA SANA, KAMTUNGUA GUARDIOLA HANA HAMU NAYE

SAMATTA AWEKA REKODI MOJA MATATA SANA, KAMTUNGUA GUARDIOLA HANA HAMU NAYE


MBWANA Samatta, nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England leo ameweka rekodi mpya kwa kufunga bao katika mechi ya fainali ya kuwania Kombe dhidi ya kikosi cha Manchester City kinachonolewa na kocha Pep Guardiola.

Mara ya mwisho aliyemfunga bao alikuwa Wayne Rooney katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2011.

Baada ya hapo, Guardiola akiwa na timu tofauti ameshiriki fainali 8 bila ya timu yake kuruhusu bao hadi Samatta kutoka Tanzania alupoliona tundu na kupachika mbao wake wa kwanza kwenye Fainali iliyochezwa Uwanja wa Wembeley.


City ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya 20 kupitia kwa Arguero na bao la pili dakika ya 30 kupitia kwa Rodri.

Bao la Mtanzania Samatta alilipachika dakika ya 41 kwa kichwa matata kilichozama nyavuni jumlajumla.

SOMA NA HII  MAKOCHA WAPIGANA MIKWARA YA HATARI LIGI YA MABINGWA