Home Habari za michezo LOMALISA ASHTUA YANGA…AFUNGUKA A-Z MPANGO WA SIRI WA YEYE KUTUA JANGWANI….

LOMALISA ASHTUA YANGA…AFUNGUKA A-Z MPANGO WA SIRI WA YEYE KUTUA JANGWANI….

Habari za Yanga

Kwa sasa beki wa kushoto wa Yanga, Joyce Lomalisa gari limewaka kutokana na kasi aliyonayo, tofauti na alivyoanza mara aliposajiliwa mwanzoni wa msimu huu na beki huyo amefunguka akianika kinachombeba, huku akiitabiria Yanga kufika mbali zaidi katika michuano ya CAF.

Beki huyo alitua Yanga akitokea FC Onze Bravos do Maquis ya Angola na kuanza kwa kusuasua kiasi kuna baadhi ya mashabiki walihisi huenda klabu hiyo imepigwa kwenye usajili wa mchezaji huyo, lakini kwa sasa jamaa amekuwa akikimbiza kiasi cha kushangaza na mwenyewe ameanika siri nzima.

Akizungumza Lomalisa alisema ubora wa kikosi cha Yanga kiliwa na malengo ndio siri iliyombeba na kumfanya aingie kwenye mfumo na kuonekana kuwa bora, huku akikiri anajiona kuwa bora zaidi kutokana na morali nzuri ya wachezaji anaocheza nao.

“Ubora wangu unatokana na namna timu inavyocheza ambayo inanilazimisha na mimi niingie kwenye mfumo kwa kufuata kile wanachokitaka nashukuru nimefanikiwa kwenye hilo,” alisema Lomalisa na kuongeza;

“Yanga ina wachezaji wengi wenye malengo sawa, hivyo ili kuweza kuingia kikosini timu itakulazimisha nawe kuendana na kile wao wanachokitaka nafurahi kwa muda nilioingia ndani ya timu hii nimeweza kuelewana na wachezaji wenzangu ikiwa ni pamoja na kuingia kwenye mfumo wa kocha.”

Lomalisa akizungumzia michuano ya kimataifa, alisema Yanga ikiwa imetinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, alisema malengo yao kama timu ni kuhakikisha wanatinga nusu fainali baada ya kufanikiwa kufuzu robo, akisema wakipambana wanaweza kutoboa na kufika mbali zaidi.

“Yanga ina kikosi kizuri imefika kwenye hatua ambayo ni mwanzo mzuri kwetu kuendeleza juhudi tulizoanzisha ili kufikia lengo hilo linawezekana kilichobaki ni benchi la ufundi kufanya kazi yao na wachezaji kufanya kwa vitendo,” alisema Lomalisa na kuongeza;

“Benchi la ufundi, wachezaji na viongozi wote unatakiwa kuwa na lengo moja ili kuweza kufanya mambo ambayo yataifanya timu kuwa bora na ya ushindani kama tulivyoanza ili tumalize pia kwa ubora.”

Alisema mchezo uliobaki ili kukamilisha makundi bado wanauchukulia kwa umuhimu zaidi ili kuhakikisha wanamaliza kundi kwa kuongoza na kuweka rekodi ambayo anaamini itadumu kutokana na timu hiyo kutoweza kufikia mafanikio hayo kwa muda.

“Aprili 2, tutakuwa ugenini kuwakabili TP Mazembe ni mchezo ambao hatutarajii mteremko tunatakiwa kujiandaa vizuri ili kwenda kusaka rekodi ya kushinda ugenini na kupata pointi tatu ambazo zitatuimarisha kileleni kwenye kundi D.” alisema Lomalisa.

SOMA NA HII  MANARA:- YANGA TUNACHEZA STAILI YA 'PPP'.....'APOROMOSHA MVUA YA MANENO' KWA NABI....