Home Uncategorized SARE MBELE YA NDANDA YAWAFUNGUA MACHO AZAM FC, LEO KUWAVAA NAMUNGO KWA...

SARE MBELE YA NDANDA YAWAFUNGUA MACHO AZAM FC, LEO KUWAVAA NAMUNGO KWA HESABU HIZI


IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa makosa waliyoyafanya kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Ndanda FC wameyafanyia kazi hivyo watawavaa wapinzani wao namungo leo kwa mtindo wa kipekee.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa matokeo ya sare yaliwaumiza kwani walijipanga kupata pointi tatu kwa kuwa sare nayo ni sehemu ya mchezo imewapa somo ambalo limewawapa mbinu mpya.

“Tulikuwa tunahitaji pointi tatu mbele ya Ndanda kwa kuwa tumepoteza na kuambulia moja hakuna tatizo tunaendelea kupambana, makosa tuliyofanya mchezo uliopita tumeyafanyia kazi.

“Mashabiki tunawaomba wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti na kutazama ni namna gani tutatoa burudani na kupata ushindi mbele ya Namungo,” amesema.

Kabla ya kumenyana na Ndanda na kulazimisha sare, Azam FC ilikubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Coastal Union, ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 45.

SOMA NA HII  10 LEO KUSAKA POINTI TATU, YANGA USIKU SIMBA JIONI, RATIBA HII HAPA