Home Habari za michezo ORUMA:- YANGA WANASHANGILIA KUPITILIZA….WAJIPONGEZE KWA KUJIFUNZA KUTOKA SIMBA…

ORUMA:- YANGA WANASHANGILIA KUPITILIZA….WAJIPONGEZE KWA KUJIFUNZA KUTOKA SIMBA…

Habari za Yanga

Ameandika Mchambuzi Nguli wa Michezo Wilson Oruma

“Nimeona Sehemu watu wanashangilia kufuzu kwa ya Yanga Africa hatua ya Robo fainali mpaka wanapitiliza

Eti viongozi wa Simba Sports Club wanatakiwa kujifunza kutoka viongozi wa Yanga. Kwenye kitu gani hasa? Mbona watu wasahaulifu kiasi hiki?

“Guys mnapo taja viongozi wa Simba mnaongelea Robo Final 3 mfululizo za CAF CHAMPIONS LEAGUE. Tena robo Final ya msimu uliopita Simba haikuwa dominant team wa Tanzania(Bingwa ligi ya Tanzania)

“Hii ni Robo Final ya kwanza ya Yanga tangu kuumbwa kwake kwa misingi ya nchi hii.

“Nafikiri busara ingetumika kuwapongeza viongozi wa Yanga kwa kujifunza kutoka kwa viongozi wa Simba na hatimaye wamejipata

“Kitu kingine nikazie tuwaheshimu matajiri sio kitu kizuri Yanga kutofika Robo final kwa miaka yote hiyo

“Nilitaka kurekebisha tu huo upotoshaji walioleta kuhusu GONGONGOWAZI”

SOMA NA HII  'KIZIZI' CHA MAYELE CHAENDELEA KUFANYA KAZI BONGO....ATUPIA TENA YANGA IKIUA MTU GOLI TISA BILA...