Home Yanga SC KATUMBI AWATIBULIA YANGA DILI LA KIUNGO MKONGO..AMWAGA MAMILIONI

KATUMBI AWATIBULIA YANGA DILI LA KIUNGO MKONGO..AMWAGA MAMILIONI


Rais na mmiliki wa TP Manzembe, Moise Katumbi ametibua mipango ya Yanga kumsajili kiungo mshambuliaji, Merceil Ngimbi Vundi.

Yanga ilikuwa inawinda saini ya mchezaji huyo mwenye miaka 24 wa klabu ya Union Maniema kabla ya TP Manzembe kumpandia dau kwenye usajili wake.

Ingawa ofisa habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amedai klabu yao haikuwa na mpango wa kumsajili kiungo huyo, habari kutoka DRC Congo zinasema klabu hiyo ilimtaka Ngimbi kuziba nafasi ya Haruna Niyonzima msimu huu wa dirisha kubwa.

Bumbuli amesema klabu yao ina mpango wa kusajili nyota wapya sita, watatu watatoka nje ya nchi na wengine watatu ni wazawa.

“Kwa Ngimbi! huyo hapana,” amesema Bumbuli ingawa habari kutoka DRC zinasema mchezaji huyo ameahidiwa dau kubwa na TP Mazembe ambalo ni zaidi ya mara mbili ya pesa ambayo Yanga walitaka kumpa, hivyo akabadili uelekeo.

“Yanga ilitaka kumpa dola $40,000 kwa mkataba wa miaka miwili, lakini TP Mazembe imekuja na dau kubwa zaidi la kama $100,000,” ilieleza taarifa kutoka Congo.

SOMA NA HII  WAKATI WATU WAKIMSIFIA KWA KUFUNGA...TAMBWE APINDISHA MDOMO KISHA AKASEMA HAYA KWA MAYELE...