Home news WAKATI WATU WAKIMSIFIA KWA KUFUNGA…TAMBWE APINDISHA MDOMO KISHA AKASEMA HAYA KWA MAYELE…

WAKATI WATU WAKIMSIFIA KWA KUFUNGA…TAMBWE APINDISHA MDOMO KISHA AKASEMA HAYA KWA MAYELE…


MSHAMBULIAJI wa DTB, Mrundi Amissi Tambwe ameiangalia kazi ya nyota wa Yanga, Fiston Mayele na kusema jamaa anatisha mbaya, lakini akamuonya asibweteke kama anataka kuweka heshima ya kuipa timu hiyo ubingwa wa ligi.

Tambwe, anayeshikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa Yanga aliyetwaa tuzo ya mabao mengi kwa nyota wa kigeni, akifanya hivyo 2015-2016 akifunga 21 na kuwa Mfungaji Bora, alisema licha ya kiwango kikubwa kinachoonyeshwa na nyota huyo, anapaswa kutambua bado ana deni kwa mashabiki wa timu hiyo.

“Wachezaji wote wanafanya vizuri, ila kutokana na nafasi yake kila mtu anamwangalia yeye, Yanga inachohitaji msimu huu ni ubingwa, sio kuangalia mafanikio binafsi hivyo jukumu lililopo mbele yake ni kupambana zaidi,” alisema Tambwe na kuongeza;

“Sina mashaka na uwezo wake, ila mashabiki wa Tanzania, ikifanya hivi leo watakusifia kesho ukikosea kidogo tu wanaanza kukuona hufai, hilo linapaswa kubaki akilini mwake ila kwa msimu huu Yanga imepata straika mkali mno.”

Mayele mwenye mabao 10 ana kazi ya kuipiku rekodi za Tambwe na Simon Msuva waliotwaa tuzo ya Mfungaji Bora mara ya mwisho kwa Yanga.

SOMA NA HII  KIFAA CHA ASEC MIMOSAS CHANUKIA YANGA...NI YULE ALIYEWAFUNGA SIMBA NNJE NDANI...ISHU IKO HIVI..