Home Habari za michezo YANGA WAIPA SIMBA UTARATIBU HUU WA KUMUAGA MKUDE UWANJANI….

YANGA WAIPA SIMBA UTARATIBU HUU WA KUMUAGA MKUDE UWANJANI….

Habari za Yanga

Klabu ya Yanga imesema kuwa iwapo watani zao Simba wanataka kumuaga kwa heshima aliyekuwa mchezaji wao, Jonas Mkude basi wajitokeze Siku ya Mwananchi, Julai 22, 2023 katika Dimba la Mkapa.

Hayo yamesemwa na Ofisa Habari Yanga, Ally Kamwe baada ya klabu ya Yanga kumsajili kiungo huyo aliyedumu Simba kwa miaka 13.

“Kama wanataka kumuona au kumuaga Mkude kwa mara ya mwisho, mahali pekee wanapoweza kuja kumuona ni kwenye kilele ya Wiki ya Mwananchi.

“Kwa hiyo kama wanataka kumuaga tunawakaribisha waje siku ya Jumamosi Julai 22, 2023 tutawapa nafasi ya kusimama na kumgia hizo salute na parade halafu tutawaruhusu watoke waende kuendelea na shughuli nyingine.

“Mkude yupo kwa ajili ya Yanga na kuwapa furaha wanayanga, ataonekana siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi pekee.

“Wengine labda wanaweza kuongea na mamlaka za wanyama pori wakamchukua Nungunungu mwingine wakampeleka kwenye tamasha lao lakini Nungunungu kwa maana ya Jonas Mkude kama wanataka kumuaga waje siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi, tunawakaribisha,” amesema Ally Kamwe.

SOMA NA HII  ANZA WIKI KWA MICHONGO YA UHAKIKA KUTOKA MERIDIANBET...HII SIO LAZIMA MKEKA AISEE...