Home kimataifa BARCELONA KUMUUZA COUTINHO KWA DAU LA HASARA

BARCELONA KUMUUZA COUTINHO KWA DAU LA HASARA


BARCELONA imeripotiwa kuwa imetoa ofa ya pauni milioni 21 kwa kiungo wao Phillipe Coutinho ambaye anawindwa na AC Milan.

Barcelona ilimnunua kiungo huyo kwa pauni milioni 143 akitokea ndani ya Liverpool lakini kiungo huyo mambo yamekuwa magumu kwake ndani ya kikosi hicho.

Hivyo atauzwa kwa dau la hasara kutokana na kushindwa kufurukuta ndani ya uwanja akiwa hapo.

Akiwa ndani ya Camp Nou alipoibukia mwaka 2018 akitokea Liverpool na msimu wa 2019/20 alipelekwa Bayern Munich kwa mkopo.

Kiungo huyo msimu uliopita alishindwa kutamba kutokana na kutumia muda mwingi kuuguza majeraha yake na msimu mzima alicheza mechi 14 na kutupia mabao matatu.

Kocha wa Barcelona Ronald Koeman yupo tayari kuachana na kiungo huyo ili kupunguza matumizi kwa kuwa hayupo kwenye mipango yake.

SOMA NA HII  AUBA AMPASUA KICHWA ARTETA