Home Uncategorized FAINALI YA KOMBE LA FA KUPIGWA SUMBAWANGA

FAINALI YA KOMBE LA FA KUPIGWA SUMBAWANGA


FAINALI ya Kombe la Shirikisho lililo mikononi mwa Azam FC mwaka huu itapigwa Sumbambawanga, mkoani Rukwa.

Uwanja huo wa Nelson Mandela kwa sasa unaendelea kufanyiwa maboresho ili fainali itakapofika uwe tayari kwa pambano hilo.

Mwaka 2019 fainali ya Kombe la FA ilipigwa Lindi na bingwa akawa Azam akishinda bao 1-0 mbele ya Lipuli likipachikwa na mshambuliaji Obrey Chirwa.

 Kwa sasa mashindano ya Kombe la Shirikisho yapo hatua ya robo fainali ambapo tayari timu nane zimeshajua zitakutana na nani kwenye mechi zao.

Azam FC ambao ni mabingwa watetezi kete yao ni dhidi ya Simba, Kagera Sugar watakutana na Yanga, Ndanda FC itakuwa dhidi ya Sahare All Stars huku Namungo  wao watakutana na Alliance FC.

SOMA NA HII  GEITA GOLD WAPANIA KUSHIRIKI LIGI KUU BARA