Home Simba SC ACHANA NA CHAMA…YANGA LEO WATAKIKOMA HIKI KIUMBE AISEE

ACHANA NA CHAMA…YANGA LEO WATAKIKOMA HIKI KIUMBE AISEE


ACHANA na Luis Miquissone, Clatous Chama ama nahodha John Bocco, kama kuna mchezaji anayewatia presha Yanga kwa sasa basi ni mtukutu, Bernard Morrison ‘BM3’. Jamaa anajua kukera na rekodi zake akianzia benchi dhidi ya timu pinzani ni wazi, Yanga ijipange kwelikweli hapo kesho.

Ndio. Kocha mkuu wa Simba Didier Gomes, mara kadhaa amekuwa akimtumia winga huyo kutoka Ghana kama mchezaji wa akiba na kumuingia kipindi cha pili na muda anaokuwepo uwanjani, jamaa amekuwa akiwachachafya mabeki na kuwatia aibu makipa wa timu pinzani.

Simba, leo itakuwa wenyeji wa Yanga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam katika mechi yao ya kiporo kilicholala Mei 8 baada ya kuahirishwa kitatanishi na kama Gomes ataamua kwenda na fomula yake ya kumuingia BM3 kutoka benchi, Jangwani inaweza kuumia naye.

Katika mechi tofauti, Morrison amethibitisha kuwa katika kikosi cha Simba kilichosheheni mastaa kibao ni ‘super sub’ kwani huwa bora zaidi akitokea benchi na kuiongezea timu makali kama alivyofanya wikiendi iliyopita mjini Songea kwenye mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

Katika mechi hiyo dhidi ya Azam, Morrison aliingizwa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mzambia Rally Bwalya na kuwatingisha mabeki wa Wanalambalamba kabla ya kuchezewa faulo dakika ya 87 na kuuanzisha mpira haraka kumpa Luis, aliyetumbukiza wavuni na kuipeleka Simba fainali.

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA NAO WAKIZIDI KUTAKATA LIGI KUU...AHMED ALLY 'KAWACHUNGULIA YANGA'..KISHA AKASEMA HAYA...