Home Uncategorized TSHISHIMBI, MOLINGA NA KABAMBA WAACHWA BONGO

TSHISHIMBI, MOLINGA NA KABAMBA WAACHWA BONGO


KIKOSI cha Yanga leo kimeanza safari kwa basi kuwafuata wapinzani wao Mwadui kwenye mchezo wa ligi utakaochezwa Juni 14, Uwanja wa Kambarage huku mastaa wake watatu wakibaki Bongo.


Mastaa waliobaki Bongo ni pamoja na Papy Tshishimbi ambaye ni nahodha, David Molinga mshambuliaji namba moja na Erick Kabamba kiungo wa Yanga.

Akizungumza na Saleh Jembe,Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wachezaji wameachwa kutokana na sababu maalumu.

“Tshishimbi amebaki kwa kuwa anaumwa, Molinga alikuwa kwenye orodha ya wachezaji yeye anajua sababu ya kubaki kwani alikuwa kwenye orodha,” amesema.

 Yanga itacheza na Mwadui, Juni 14 Uwanja wa Kambarage.
SOMA NA HII  WATU WAENDELEA KUCHOTA MKWANJA NDANI YA SPORTPEA, CHALII AONDOKA NA MILIONI 6 NA USHEE