Home Uncategorized MOLINGA AACHWA BONGO,HIKI HAPA AMESEMA

MOLINGA AACHWA BONGO,HIKI HAPA AMESEMA

KIKOSI cha Yanga leo kimeanza safari ya kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui utakaochezwa Juni 14.

Katika kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Msaidizi, Charles Mkwassa, mtupiaji namba moja David Molinga ameachwa Bongo huku habari zikieleza kuwa amegoma jambo ambalo amelikanusha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, David Molinga ameandika:- Nataka nikanushe hii habari kwamba nimegoma kusafiri na team kwanza nimewakumbushe kitu cha peke imenileta Tanzania ni mpira na kazi yangu ndio iyo sasa iko ivi tangu team imeanza mazoezi sijawahi kukosa na nafata program za mwalim vizuri.

” Lakin jana list (orodha) ilitoka na mimi jina langu halijakuwepo sasa itasemekana vipi mimi nimegoma kama ndio ivyo muulizeni coach ndio alitaja list (orodha) yake imekuwa tabia kila mara kila kitu mimi tu ata kama sjafanya kitu kibaya utaskia tu Molinga ‘this is too much’ (hii imezidi).

SOMA NA HII  WAGENI 100 WAIGOMBANIA NAFASI YA AMMUNIKE, WAZAWA WAICHUNIA