Home Uncategorized GEITA GOLD WAPANIA KUSHIRIKI LIGI KUU BARA

GEITA GOLD WAPANIA KUSHIRIKI LIGI KUU BARA

UONGOZI wa Geita Gold, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza umesema kuwa mipango yao ni kuona wanatimiza malengo yao ya kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao kwa kupambana kwenye mechi zao wanazocheza.

Geita Gold ipo Kundi B ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 16 na ina pointi 26, kinara wao wa kucheka na nyavu ni George Mpole ambaye amefunga mabao nane na katika mabao hayo ana hat trick moja aliyofunga mbele ya Pamba Sports Club mchezo uliochezwa Uwanja wa Nyankumbu Sekondari.

Ofisa Habari wa Geita Gold, Gabriel Nyasilu, maarufu kama Gabo amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wachezaji wanapambana kuona wanafikia malengo waliyojiwekea.

“Ni kazi kubwa na ushindani upo ila tunahitaji kuona malengo yetu ya kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao yanatimia, mashabiki watupe sapoti,” amesema,
SOMA NA HII  MARTIAL ASEPA NA MPIRA WAKE JUMLA WAKIIPA KICHAPO CHA MABAO 3-0 SHEFFIELD